Tuesday, August 30, 2016

MAHOJIANO NA PROF JULIUS NYANG'ORO

Profesa Julius Nyang'oro ni Mwalimu, mtaalam wa sayansi ya siasa na mwanasheria.

Amekuwa mwalimu tangu mwaka 1977 nchini Tanzania na hapa nchini Marekani.

Ni mwandishi wa vitabu zaidi ya 14, vingi vikiigusia Tanzania kwa namna moja ama nyingine. Moja ya vitabu alivyoandika, na ambavyo vilimtambulisha zaidi kwa jamii ya waTanznia, ni kumhusu Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete. Ambapo ameandika vitabu viwili kumhusu.

Prof Nyang'oro alikuwa mkarimu sana kuungana nasi kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU Jumatatu ya Agosti 29, 2016 kuzungumzia mambo mbalimbali kuihusu Tanzania akiwa mwandishi, mwalimu, mtaalamu wa mausala ya siasa na mwanasheria
KARIBU

DAR ES SALAAM:ANGEL MAGOTI ALIVYOIMBA KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA NDOA YA RAIS MSTAAFU WA TANZANIA BENJAMINI MKAPA


Mwimbaji wa Nyimbo za Injili nchini Tanzania Angel Magoti (Picha ya Kwanza) hivi karibu alipata nafasi ya kuimba kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya ndoa ya Rais Mstaafu wa Tanzania wa awamu ya tatu  Benjamin Mkapa ambayo pia ilihudhuriwa na marais wastaafu,Mawaziri Wakuu Wastaafu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli

Katika tukio hilo Angel Magoti aliimba nyimbo sita.

Friday, August 26, 2016

DAR ES SALAAM:WAIMBAJI WA THE LIGHT BEARERS WAREJEA NCHINI TANZANIA TOKA UINGEREZA

 
 
 
 
 
Waimbaji 14 wa The Light Bearers ambao walisafiri kuelekea Reading,Nchini Uingereza kwa mkutano wa Injili ulioendeshwa na Mch Baraka Butoke toka Tanzania ambao ulikuwa umeandaliwa na Kanisa la Waadventista Wa Sabato Angaza la mjini humo ambako walikuwa huko kwa takribani majuma matatu.

The Light Bearers wamewasili saa saba mchana ya ijumaa ya Agosti 26,Mwaka huu katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam ambapo walipokelewa kwa kupewa zawadi ya maua na keki iliyoandaliwa na Kundi la Whatsapp la Marafiki wa Light Bearers ambalo imekuwa likishiriki kuratibu baadhi ya matukio ya waimbaji hao nchini na nje ya Tanzania.

Wakiwa nchini Uingereza waimbaji hao  wamefanikiwa kurekodi santuri mwonekano namba 3 na 4 ambazo nyimbo zake mbili mpya zimeshaanza kuoneshwa katika vituo vya televisheni na kwenye mitandao,pia walitembelea ofisi za Konferensi,Unioni na Divisheni zilizoko nchini humo.

Monday, August 22, 2016

DAR ES SALAAM:WAIMBAJI WA KWAYA YA UBUNGO HILL WAFUNGA NDOA

Jana ilikuwa ni siku ya  kihistoria kwa waimbaji wawili wa Kwaya ya Waadventista ya Ubungo Hill jijini Dar es salaam, Eliezer na Dorah kwa kufunga pingu za maisha kwenye  ibada ilifanyika katika kanisa hilo.Huku hafla ya kuwapongeza ikifanyika katika Ukumbi wa Law School, Mawasiliano jijini Dar Es Salaam.
 

Monday, August 15, 2016

NAIROBI:MKUTANO WA MAKAKATI KAZI WA MAWASILIANO WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO WAANZA JIJINI NAIROBI


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani Costa Williams


Baadhi ya wajumbe toka Tanzania


 Mkutano wa Mkakati kazi  Wa Idara ya Mawasiliano katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato katika kanda ya Africa Mashariki na Kati (ECD) unaohusisha viongozi Wa Idara hiyo pamoja na Vituo vya Habari vya Habari umeanza hii Leo jijini Nairobi nchini Kenya. 

Mkutano huo unaowaunganisha Wakurugenzi Wa Idara ya Mawasiliano pamoja na wasimamizi Wa vituo vya habari vya kanisa katika kanda hiyo unaongozwa Na Mkurugenzi Wa Idara hiyo katika ngazi ya Ulimwenguni Costa Williams. 

Williams amesisitiza juu ya matumizi ya maneno katika injili kupitia mitandao ya kijamii,Redio,Televishen na katika Mazungumzo na namna ya kukabiliana na Majanga katika kanisa. Lengo kuu la mkutano huo ni kupanga mikakati ya kanisa kupitia Idara ya mawasiliano kwa miaka 5.

DAR ES SALAAM:KIPINDI CHA LULU ZA INJILI CHA MORNING STAR RADIO NA TV KILIVYORUKA LIVE TOKA MAGOMENI MWEMBECHAI

ARUSHA: THE GOLDEN GATE WAKO SAKINA JIJINI ARUSHA KWA MAKAMBI MWALIMU WAO AMEZUNGUZIA UJIO HUO

 

Waimbaji 21 wa Kwaya ya The Golden Gate toka Kampala Uganda ambayo imedumu kwa miaka zaidi ya 40 wako kwenye Makambi ya Sakina jijini Arusha ambayo yalianza Agosti 13 na kutarajiwa kumalizika Agosti 20 mwaka huu.

Idadi hiyo ya waimbaji inajumuisha waimbaji waliokuwepo toka kwaya hiyo inaanzishwa.

Miongoni mwa Video ya waimbaji hao ambayo imeonekana kusambazwa na watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii hasa WhatsApp ni ile ya wimbo wao wa zamani wa Twaimba Tumejaa Furaha waliyoiimba kwenye mkutano huo hivi karibuni.

Yafuatayo ni Mahojiano na Mwalimu na Mwimbaji wa Kwaya ya The Golden Gate Muanika Samweli Kigozi

WANAOIFUATILIA

 

MTANGAZAJI. Copyright 2011 All Rights Reserved This Blog presented by ReedzSolution